وَٱلضُّحَىٰ
Naapa kwa mchana!
Soma na usikilize Ad-Dhuhaa, sura ya 93, yenye aya 11. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلضُّحَىٰ
Naapa kwa mchana!
وَٱلَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ
Na kwa usiku unapo tanda!
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
وَلَلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ ٱلْأُولَىٰ
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰٓ
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَـَٔاوَىٰ
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
وَوَجَدَكَ ضَآلًّا فَهَدَىٰ
Na akakukuta umepotea akakuongoa?
وَوَجَدَكَ عَآئِلًا فَأَغْنَىٰ
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
فَأَمَّا ٱلْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ
Basi yatima usimwonee!
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنْهَرْ
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.