أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
Soma na usikilize Al-Maa'un, sura ya 107, yenye aya 7. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
فَذَٰلِكَ ٱلَّذِى يَدُعُّ ٱلْيَتِيمَ
Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
Wala hahimizi kumlisha masikini.
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ
Basi, ole wao wanao sali,
ٱلَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
Ambao wanapuuza Sala zao;
ٱلَّذِينَ هُمْ يُرَآءُونَ
Ambao wanajionyesha,
وَيَمْنَعُونَ ٱلْمَاعُونَ
Nao huku wanazuia msaada.