ٱلْقَارِعَةُ
Inayo gonga!
Soma na usikilize Al-Qaari'a, sura ya 101, yenye aya 11. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱلْقَارِعَةُ
Inayo gonga!
مَا ٱلْقَارِعَةُ
Nini Inayo gonga?
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْقَارِعَةُ
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
يَوْمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلْفَرَاشِ ٱلْمَبْثُوثِ
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ ٱلْمَنفُوشِ
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٌ
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا هِيَهْ
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
نَارٌ حَامِيَةٌۢ
Ni Moto mkali!