أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ
Hatukukunjulia kifua chako?
Soma na usikilize Ash-Sharh, sura ya 94, yenye aya 8. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ
Hatukukunjulia kifua chako?
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ
Na tukakuondolea mzigo wako,
ٱلَّذِىٓ أَنقَضَ ظَهْرَكَ
Ulio vunja mgongo wako?
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ
Na tukakunyanyulia utajo wako?
فَإِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا
Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
إِنَّ مَعَ ٱلْعُسْرِ يُسْرًا
Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
فَإِذَا فَرَغْتَ فَٱنصَبْ
Na ukipata faragha, fanya juhudi.
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرْغَب
Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.