أَلْهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ
Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
Soma na usikilize At-Takaathur, sura ya 102, yenye aya 8. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلْهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ
Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
حَتَّىٰ زُرْتُمُ ٱلْمَقَابِرَ
Mpaka mje makaburini!
كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ
Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ
Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ ٱلْيَقِينِ
Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
لَتَرَوُنَّ ٱلْجَحِيمَ
Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ ٱلْيَقِينِ
Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
ثُمَّ لَتُسْـَٔلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ
Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.