وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيْتُونِ
Naapa kwa tini na zaituni!
Soma na usikilize At-Tin, sura ya 95, yenye aya 8. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِّسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيْتُونِ
Naapa kwa tini na zaituni!
وَطُورِ سِينِينَ
Na kwa Mlima wa Sinai!
وَهَـٰذَا ٱلْبَلَدِ ٱلْأَمِينِ
Na kwa mji huu wenye amani!
لَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ فِىٓ أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ
Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
ثُمَّ رَدَدْنَـٰهُ أَسْفَلَ سَـٰفِلِينَ
Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِٱلدِّينِ
Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَحْكَمِ ٱلْحَـٰكِمِينَ
Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?