إِذَا زُلْزِلَتِ ٱلْأَرْضُ زِلْزَالَهَا
Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
Soma na usikilize Az-Zalzala, sura ya 99, yenye aya 8. Iliteremshwa Madina. Maandishi asilia ya Kiarabu yenye tafsiri zilizothibitishwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا زُلْزِلَتِ ٱلْأَرْضُ زِلْزَالَهَا
Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
وَأَخْرَجَتِ ٱلْأَرْضُ أَثْقَالَهَا
Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
وَقَالَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَا لَهَا
Na mtu akasema: Ina nini?
يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا
Siku hiyo itahadithia khabari zake.
بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا
Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ ٱلنَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا۟ أَعْمَـٰلَهُمْ
Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُۥ
Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُۥ
Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!