فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَـٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ
Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
Soma Ukurasa 577 kwa kutumia mipaka iliyohakikiwa ya Tanzil. Aya 28 katika sehemu hii.
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَـٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ
Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
فَمَا لَهُمْ عَنِ ٱلتَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ
Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ
Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍۭ
Wanao mkimbia simba!
بَلْ يُرِيدُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً
Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ
Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذْكِرَةٌ
Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anaye taka atakumbuka.
وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ ٱلتَّقْوَىٰ وَأَهْلُ ٱلْمَغْفِرَةِ
Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
لَآ أُقْسِمُ بِيَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ
Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
وَلَآ أُقْسِمُ بِٱلنَّفْسِ ٱللَّوَّامَةِ
Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
أَيَحْسَبُ ٱلْإِنسَـٰنُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُۥ
Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُۥ
Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
بَلْ يُرِيدُ ٱلْإِنسَـٰنُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُۥ
Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
يَسْـَٔلُ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلْقِيَـٰمَةِ
Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
فَإِذَا بَرِقَ ٱلْبَصَرُ
Basi jicho litapo dawaa,
وَخَسَفَ ٱلْقَمَرُ
Na mwezi utapo patwa,
وَجُمِعَ ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ
Na likakusanywa jua na mwezi,
يَقُولُ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ ٱلْمَفَرُّ
Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
كَلَّا لَا وَزَرَ
La! Hapana pa kukimbilia!
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ ٱلْمُسْتَقَرُّ
Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
يُنَبَّؤُا۟ ٱلْإِنسَـٰنُ يَوْمَئِذٍۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
بَلِ ٱلْإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفْسِهِۦ بَصِيرَةٌ
Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
لَا تُحَرِّكْ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِۦٓ
Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُۥ وَقُرْءَانَهُۥ
Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
فَإِذَا قَرَأْنَـٰهُ فَٱتَّبِعْ قُرْءَانَهُۥ
Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُۥ
Kisha ni juu yetu kuubainisha.