أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَـٰبِ ٱلْفِيلِ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
Soma na usikilize Al-Fil, sura ya 105, yenye aya 5. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَـٰبِ ٱلْفِيلِ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?
أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِى تَضْلِيلٍ
Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ
Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,
تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ
Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍۭ
Akawafanya kama majani yaliyo liwa!