وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ
Ole wake kila safihi, msengenyaji!
Soma na usikilize Al-Humaza, sura ya 104, yenye aya 9. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ
Ole wake kila safihi, msengenyaji!
ٱلَّذِى جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُۥ
Aliye kusanya mali na kuyahisabu.
يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخْلَدَهُۥ
Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!
كَلَّا ۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِى ٱلْحُطَمَةِ
Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحُطَمَةُ
Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama?
نَارُ ٱللَّهِ ٱلْمُوقَدَةُ
Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.
ٱلَّتِى تَطَّلِعُ عَلَى ٱلْأَفْـِٔدَةِ
Ambao unapanda nyoyoni.
إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ
Hakika huo utafungiwa nao
فِى عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍۭ
Kwenye nguzo zilio nyooshwa.