تَبَّتْ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
Soma na usikilize Al-Masad, sura ya 111, yenye aya 5. Iliteremshwa Makka. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
تَبَّتْ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ
Atauingia Moto wenye mwako.
وَٱمْرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلْحَطَبِ
Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
فِى جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍۭ
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.