إِذَا جَآءَ نَصْرُ ٱللَّهِ وَٱلْفَتْحُ
Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,
Soma na usikilize An-Nasr, sura ya 110, yenye aya 3. Iliteremshwa Madina. Maandishi asilia ya Kiarabu kutoka Tanzil yenye tafsiri zilizohakikiwa.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا جَآءَ نَصْرُ ٱللَّهِ وَٱلْفَتْحُ
Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,
وَرَأَيْتَ ٱلنَّاسَ يَدْخُلُونَ فِى دِينِ ٱللَّهِ أَفْوَاجًا
Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,
فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَٱسْتَغْفِرْهُ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ تَوَّابًۢا
Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.